upande.jpg_480_480_0_64000_0_1_0.jpg

UPANDE MMOJA

Haya mapenzi ya upande mmoja
Yananimaliza miye
Mbona mwenzangu nikupe moyo wangu
Kisha miye niumie
Yananiuma, yananiuma
Yananiuma tena kwa sana
Eee-eee
Laiti ningalijua
Laiti ningefichua
Ningalijua nisingalikupenda ewe paka wa mwitu
Ningefichua moyo wako paka ningejua we si mtu
Uuuuu

Umenifanya kuwa mjinga
Ukanigeuza mzinga
Ukachovya yangu yote mapenzi ukaniacha bure
Umeutoboa moyo wangu ili kifua kifure
Mapenzi yote yamemwagika
Sina hata tone hakika
Hakika... Hakika

Lakini dunia kandanda
Sikiza hiki kinanda
Ulinitia kidonda hujui utageuzwa nzi
Utatimuliwa malishoni utamani kurudi zizi
Moyo nitakua nishaushona
Machozi yako sitayaona
Mpenzi... mpenzi

© Februari, 2015